Aliyekuwa mhadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini, Prof. Mwesiga Baregu amefariki dunia.
Prof. Baregu pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Ni Profesa Mwandamizi aliyehudumu muda wake wote wa utumishi Chuo Kikuu cha Dsm, na alipostaafu akaenda Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania, SAUT.
Amekuwa maarufu kutokana na Ushiriki wake kwenye mijadala ya Kisiasa nchini Tanzania.
Alikuwa mmoja wa wajumbe wa tume ya Katiba ya Warioba na Mwaka 2005 alipitishwa na Chadema kugombea Urais wa Tanzania lakini baadae alijitoa kuwania nafasi hiyo badala yake Chadema wakamuweka Mbowe agombee.
Kupitia ukurasa wa Twitter Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo amesema, “pumzika kwa amani Profesa Baregu. Mmoja wa wasomi walioamini kuwa huwezi kutenganisha taaluma na siasa. Ulitufundisha baadhi yetu tunaokubali msimamo huo wasomi wanaweza kufanya siasa bila kupoteza sifa zao.”
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika ”mapumziko mema Profesa Baregu”.
Ni Profesa wa Sayansi ya Siasa.