Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imeendelea ‘kupiga jeki’ miradi mingi ya kimaendeleo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Miongoni mwa maeneo hayo ni pamoja na yale ya Vijijini ambayo yamekuwa yakifurahia shughuli na uwepo wa Uhifadhi na utalii katika maeneo yanayowazunguka.
Hadi sasa, jumla ya shilingi 340,301,000 imekwisha tumika kusaidia ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule 10, Vituo vya afya 3 Visima vya wananchi 14 mabwawa ya uvuvu 2, ukarabati wa soko la samaki na kusaidia vikundi katika shughuli zao.
Miongoni mwa maeneo yaliyonufaika ni pamoja na Kondoa (ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa Zahanati za Idindiri, Mauno, Bomangombe na Ihari), Kibondo, Kaliua, Bunda, Kilwa, Kilwa, Masasi, Njinjo, Napacho na Masuguru.