Serikali imeagiza mtambo mkubwa wenye uwezo wa kukagua magari 1,152 kwa siku ili kudhibiti magari mabovu yanayoingia kutoka nje ya nchi.
Mtambo huo unatarajiwa kuwasili nchini mwezi Julai, 2021 umeagizwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Hayo yamebainishwa na Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Diocles Ntamulyango akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambapo amesema mtambo huo ulioagiziwa nchini Ujerumani unagharimu shilingi bilioni tatu.
“Mtambo mtambo huo utakuwa na uwezo wa kukagua magari 48 kwa saa moja, utakarahisisha ufanisi na kufanyika kwa kasi kubwa. Kwa mwezi tunatarajia kukagua magari 34560 na kwa mwaka agari 414,720” amesema Ntamulyango.