Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jones Kilimbe amesema kuwa lengo la serikali kuboresha sera na kanuni za mitandao ya kijamii ni kutaka kuweka usalama katika nchi pamoja na kutumiwa vyema ili iweze kuleta maendeleo.
Ameyasema hayo wakati akifunga warsha na vyombo vya habari vya mtandaoni na kusisitiza kuwa kutokana na ukuaji wa mitandao ya kijamii ni bora ikatumika vizuri kwa kuzingatia utu na staha.
Amesema kuwa kutokana na ukuaji wa mitandao ya kijamii umeweza kuonyesha jinsi teknolojia ilivyopokelewa vizuri kwani taarifa zinapatikana kwa haraka zaidi endapo ukiwa na simu ya mkononi.
“Kutokana na mapokeo mazuri inabidi mitandao hii itumiwe vizuri kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa. Pia nashauri iwepo sera na kanuni za kufanikisha mitandao hii itumike vyema kimaendeleo na ndiyo maana serikali imeamua kuja na maboresho ambayo yatakuwa bora na salama, pia TCRA itakuwa bega kwa bega,”amesema Dkt. Kilimbe
-
Wenye vyeti feki kurejesha mishahara waliyolipwa
-
Wivu wamponza mke atiwa mbaroni
-
Mbarawa atoa agizo baraza la Ujenzi
Hata hivyo, Dkt. Kilimbe ameongeza kuwa kutokana na ukuaji wa mitandao ya kijamii umeweza kuonyesha jinsi teknolojia ilivyopokelewa vizuri kwani taarifa zimeweza kupatikana kwa haraka zaidi.