Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki katika mkutano na watumishi amewatahadharisha wenye vyeti feki ambao bado hawajatambuliwa kuwa endapo watabainika na vyeti feki mara baada ya zoezi ilo kuishi watalazimika kurejesha mishahara yote waliolipwa

Hivyo amewataka watumishi wa umma wanaoendelea kutumia vyeti feki wajiondoe wenyewe kazini.

Aidha amesema kuwa pamoja na zoezi hilo la kuhakiki watumishi wa umma kuendelea bado kazi hiyo imekuwa na dosari kwani bado kunawatumishi wanaendelea kutumia vyeti feki.

Hivyo amewataka Makatibu Tawala wa Mkoa kuangalia na kujiridhisha na majina ya watumishi kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi wa umma na kwenye kazi ya uhakiki kama yanafanana.

”Majina yalioonekana kwenye zoezi la uhakiki  yanapaswa kuonekana kwenye orodha ya malipo ya mishahara na kama kuna mtumishi hajahakikiwa anatakiwa aondolewe kwenye malipo ya mshahara,” amesesma Kairuki.

Hayo yamezungumzwa mapema jana kwenye mkutano na watumishi wa Halmashauri za Kibaha Mjini, Vijijini na watumishi wa mkoa wa Pwani, baada ya kazii ya kuhakiki vyeti iliyofanywa mkoani pwani.

 

 

 

Huu ndio wimbo unaomkera Lukaku
Video: Serikali yavunja ukimya suala la Tundu Lissu