Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema Serikali ya awamu ya sita imewainua wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa za kiteknolojia na mikopo yenye masharti nafuu ili waweze kupambana na ukatili wa kijinsia.
Dkt. Gwajima, ameyasema wakati wa Mkutano Mkuu wa tano wa Mwanamke Kiongozi kwa mwaka 2023 uliofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
“Serikali ya awamu ya sita imewainua wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa za kiteknolojia na mikopo yenye masharti nafuu ili waweze kupambana na ukatili wa kijinsia,” amema Waziri Dkt. Gwajima.
Hata hivyo amebainisha kuwa, Serikali imeratibu programu ya kuwezesha wanawake katika maendeleo na mwelekeo wa kidijitali ili wafahamu masuala ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu.