Takribani watu 130,000 wanakabiliwa na baa la njaa katika Pembe ya Afrika, huku Shirika la Afya Duniani – WHO likionya kuwa maisha ya watu yamo hatarini kwa kuweza kufikwa na umauti au maradhi kwa jamii.

WHO, imetoa tahadhari hiyo huku ikisema watu wapatao milioni 48 kwenye nchi za Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini na Uganda wanakabiliwa na viwango vikubwa vya ukosefu na uhaba wa chakula.

Meneja matukio wa Shirika la WHO wa Pembe ya Afrika , Liesbeth Aelbrecht amesema watu hao wanakabiliwa na njaa huku hatari ya magonjwa na vifo vikiwanyemelea na kutaka nchi wahisani kuhakikisha wanachukua hatua za dharula kusaidia hatua hiyo.

Mabadiliko ya hali ya hewa yameleta athari eneo kubwa la pembe ya Afrika. Picha ya The Globe post.

Aelbrecht ambaye alikuwa akiongea na Waandishi Habari mjini Geneva kwa njia ya video kutoka Nairobi, ameongeza kuwa kati ya watu 129,000, watu 96,000 kati yao wapo nchini Somalia na 33,000 katikia Taifa la Sudan Kusini.

Ameongeza kuwa, maeneo mengi katika ukanda huo yanapambana na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 40, huku yakiathiriwa kwa mafuriko na kwamba ongezeko la miripuko ya magonjwa limeshuhudiwa na idadi kubwa ya watoto wenye utapiamlo.

Teknolojia, mikopo nafuu yasaidia mapambano ukatili wa kijinsia
Program Mwanamke Kiongozi itumike kuibua vipaji: Waziri SMZ