Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi lililoikumba Uturuki na Syria, imeongezeka kwa mara nyingine na kufikia watu 21,000.

Waokoaji katika tukio hilo wanasema wanatarajia huenda idadi hiyo ikaongezeka, kutokana na hali ya baridi kali nchini Uturuki inayoonekana kulemaza shughuli za uokoaji na kutishia maisha ya maelfu ya manusura waliopoteza makazi.

Simanzi.

Aidha, wakati juhudi za uokoaji zikiendelea maelfu ya manusura wamehamishwa kutoka katika miji iliyoathirika zaidi nchini Uturuki, huku raia katika miji nchini Syria wakisaidia kuwazika wenzao waliopoteza maisha.

Hata hivyo, mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekosoa muda ambao umoja wa mataifa ulichukuwa kutuma msaada Kaskazini Magharibi mwa Syria, wakati ambapo mataifa ya China na Marekani yameahidi tena kutoa msaada.

Majaliwa: Wizara, Taasisi zingatieni vipaumbele vya maendeleo
Watakao wazuia Wanafunzi kwenda shule kukiona: Serikali