Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya Vituo vya kazi kwa mabalozi wawili, ambapo Humphrey Polepole sasa anakuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kabla ya mabadiliko hayo alikuwa akihudumu kama Balozi wa Tanzania Nchini Malawi.

Aidha, katika mabadiliko hayo pia Rais Samia amempangia Balozi Luteni Jenerali mstaafu Yacoub Mohamed kuiwakilisha Tanzania katika Falme za Kiarabu – UAE, ambapo kabla ya mabadilko hayo Balozi Luteni Jenerali Mstaafu, Yacoub Mohamed alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki.

Tanzania kushirikiana na WHO kanuni za Afya Kimataifa
FC Barcelona na simulizi za Ilkay Gundogun