Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepanga kuwafungulia mashataka watu waliosambaza ujumbe ambao sio wa kweli kwenye mitandao ya kijamii kufuatia taarifa walizokuwa wanazisambaza zikidai kuwa shirikisho hilo limeongeza posho za vikao.
Akizungumza na wanahabari leo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema kuwa, amaelazimika kutoa ufafanuzi huo kufuatia hivi karibuni kuwepo kwa taarifa hizo zilizosambaa na kuwa hazina ukweli wowote.
Alisema katika taarifa hizo walidai kuwa TFF imeongeza posho kwenye vikao vinavyofanywa na kamati ya utendaji huku kwa mwezi wakipokea kiasi cha milioni m Mbali na hilo, taraifa hiyo ilieleza kuwa Rais wa TFF, Wallace Karia anapokea kiasi cha milioni 6 wakati makamu wale Richard Wambura, akilamba milioni 5 kwa mwezi kama malipo ya kazi yao.
Kidau alisema kuwa, tayari hadi sasa wameshapata majina ya watu 10 ambayo wanaendelea kufuatilia na wengine na baada ya hapo watawafungulia mashtaka.
“Kuna taarifa ambazo si za kweli watu wanazisambaza kwenye mitandao ya Kijamii na sasa hivi kuna sheria za mitandao, leo baada ya kikao hiki tunaenda kuwafungulia mashtaka watu waliohusika na jambo hili kwa kueneza vitu ambavyo sio vya kweli,” amesema Kidao.
Alisema wataendelea kufuatilia kila mtu aliyehusika kwa maana ya aliyetuma ujumbe huo kwani kwa sasa wanazo baadhi ya namba na watazichapisha.oja kila mmoja kwaajili ya mishahara.