Shirikisho la Soka Tanzania TFF limejibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuitaka Tanzania isusie kucheza mechi na Libya ili kupinga vitendo vya biashara ya utumwa inayoendelea nchini humo.
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa suala hilo ni nyeti na limefikishwa katika uongozi wa juu na kwamba litatolewa majibu hivi karibuni.
“Msimamo utatolewa na viongozi wangu mara baada ya kukaa na kutafakari hali halisi kwa sasa, na wenye uwezo wa kukaa na kutafakari ni viongozi wa juu, itakapokuwa tayari mtajulishwa,” amesema Lucas
Aidha, Zitto ametoa wito kwa TFF kuitaka timu ya Kilimanjaro Stars isusie mechi inayotarajiwa kuchezwa na Libya, ili kuonyesha kutokubaliana na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuendeleza biashara ya utumwa.