Shirikisho la Soka nchini ‘TFF’ limefafanua kuwa adhabu aliyopewa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Fredrick Mwakalebela kuwa imeegemea kwenye upande wake wa uongozi wa klabu na si kwenye masuala mengine ya kama vile kumzuia asifuatilie taarifa za michezo.
Mwakalebela alitoa shutuma hizo mwishoni mwa juma lililopita alipohojiwa na moja ya chombo cha habari jijini Dar es salam, ambacho kilitaka kufahamu kauli yake baada ya adhabu yake kutangaza na kamati ya Madili ya TFF.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya TFF Clifford Mario Ndimbo amesema kama taarifa ilivyoeleza, ni dhahir Mwakalebela alikua na sababu za kuingia kwenye tuhuma za kukosa maadili, baada ya kutangaza mamboa mbayo alishindwa kuyatolewa ushahidi.
“Kama ambavyo taarifa ya adhabu ilivyosema, na ni tofauti na alivyoielezea kwamba haruhusiwi hata kusoma magazeti au ikifika kwenye taarifa za michezo azime TV asiangalie. Adhabu aliyopewa ni kwamba majukumu yake ambayo amekuwa nayo ndipo aadhabu ilipoegemea.” amesema Ndimbo
“Asijihusishe na majukumu hayo ya kiuongozi kwa muda huo ila mengine kuhusu kutokusoma magazeti labda alikuwa anafurahisha genge tu.”
“Linapokuja suala la kwenda uwanjani hilo sio kujishugulisha na suala la uongozi wa mpira na maana yake umekwenda kama mtazamaji mwingine.” Amesema Ndimbo
Hii ni taarifa ambayo ilitolewa na TFF kuthibitisha adhabu ya Mwakalebela mnamo April 02.