Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema hii leo limeipongeza Klabu ya Simba kwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF), ikiwa ni siku chache baada ya kuibanjua AS Vita Club ya DR Congo mabao 4-1.

Akitoa pongezi hizo bungeni jijini Dodoma, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alisema kuna wabunge yawezekana hawajaelewa uzito wa ushindi huo wa Simba.

“Ni jambo ambalo sisi kama taifa tunapaswa kuungana kuwatia moyo wachezaji wetu na klabu yetu iendelee kufanya vizuri kwa sababu inapata fursa ya kuitangaza nchi yetu vizuri,” alisema.

Dk.Tulia alisema “Naamini mashabiki wa Yanga wataungana nami katika pongezi hizi kwa klabu ya Simba.”

Simba SC imeshakata tiketi ya kucheza Hatua ya Robo Fainali, huku ikongoza msimamo wa kundi A kwa kufikisha alama 13, iifuatiwa na Al Ahly ya Misri yenye alama 8, AS Vita Club inashika nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 4 na Al Merrikh inaburuza mkia kwa kumiliki alama mbili.

CAG: Deni la Taifa linaongezeka kwa kasi
Sanga: Simba SC bingwa 2020/21