Kuelekea mwishoni mwa dirisha dogo la usajili, Shirikisho la Soka la nchini TFF, limetoa angalizo kwa klabu juu ya usajili wa wachezaji wao.
Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa, kuna tatizo ambalo klabu limekuwa likilifanya kwa kuwaruhusu wachezaji kuondoka dakika za mwisho za usajili.
Amesema suala hilo limekuwa likiharibu maisha ya wachezaji ambapo amesema kuwa ni vema kama klabu haina mpango na wachezaji kadhaa ni bora ikawaruhusu mapema kuliko kusubiri dakika za mwisho kisha wachezaji wanakuwa katika wakati mgumu.
-
TFF yatoa agizo kwa timu za Simba na Yanga
-
Joseph Kimwaga, Shaaban Iddy waendelea kupambana na hali zao
Lucas amesema kanuni za usajili zinaruhusu mchezaji kufanya mazungumzo miezi sita ya mwisho ya mkataba, hivyo ni vema suala hilo likazingatiwa.
Licha ya kutotaja majina ya klabu au wachezaji, lakini mara kadhaa imetokea wachezaji wa timu za Simba na Young Africans ndiyo ambao wamekuwa wakiingia katika matatizo ya kimkataba ya kuachwa dakika za mwisho.