Kamishna Mkuu wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo amesema wakati umefika kwa nchi zilizoendelea, kuweka mchango wao kwa nchi zinazoendelea kupunguza gesi joto.
Prof. Silayo ameyasema hayo, wakati wa hafla ya hafla ya kusaini hati ya makubaliano kati ya kampuni hiyo na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), kuhusu biashara ya kaboni iliyofanyika jijini Dodoma.
Amesema, hatua ya kusaini makubaliano na Blue Carobon ni mwanzo wa utekelezaji wa shughuli hizo na kampuni hiyo itaanza mchakato wa kusajili, kwa kuzingatia maelekezo.
Aidha, ametoa msukumo kwa nchi zinazoendelea kuweka kipaumbelea katika kuhifadhi mistu ili kuweka msingi wa maeneo yanayoweza kujikita katika biashara ya kaboni ambayo imeshakuwa ni mbadala wa shughuli za kiuchumi hivi sasa.