Rapa The Game ameshushiwa rungu la kisheria baada ya Jaji kumtaka amlipe pesa ndefu mrembo aliyemshtaki kwa kumnyanyasa kingono.

Kwa mujibu wa TMZ, Jaji amemuamuru rapa huyo kumlipa mtangazaji mrembo wa ‘reality show ya She’s Got Game’, Priscilla Rainey kiasi cha dola za Kimarekani milioni 7.13 ($7.13 Million).

Katika kesi ya msingi, mrembo huyo alitaka mahakama imuamuru rapa huyo wa ‘Hate it or Love It’ amlipe dola za kimarekani milioni 10 ($10 million).

Taarifa zailizoripotiwa na TMZ zimeeleza kuwa rapa huyo amepanga kukata rufaa akipinga maamuzi hayo.

Justin Bieber apiga mazoezi na Neymar, atulia na Messi, Suarez
NEMC yaipiga faini ya mil. 15 halmashauri ya Kahama