Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini, NEMC limeipiga faini ya shilingi milioni kumi na tano Halmashauri ya wilaya ya Kahama kwa kile kinachodaiwa ni uzembe wa kuto zingatia sheria ya mazingira kwa kuliweka Dampo la mji huo katika hali hatarishi kwa mazingira na viumbe hai.

Katika Ziara ya Naibu Waziri Mpina Leo Mjini Kahama, iliyohusisha ukaguzi wa Dampo, machinjio viwanda na soko la mjini kahama kumebainika kuwa na uzembe kwa watendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama, wa kutosimamia utupwaji wa taka katika Dampo la mji huo.

Kufuatia ukiukwaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake, Baraza la mazingira nchini  NEMC limeshawishika kuitoza faini Halmashauri hiyo ya shilingi milioni kumi na tano na kutakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili.

Ziara ya Naibu Waziri  Mpina wilayani Kahama ni Muendelezo wa Ziara zake nchini za ukaguzi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

The Game ‘apigwa rungu’ kwa unyanyasaji wa kingono
Video: Bodaboda sasa ni janga - Jeshi la Polisi