Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini imekanusha kutokea kwa hali ya Kimbunga “ELIAKIMU” katika maeneo yanayozunguka nchi na kudai Kimbunga hicho kipo kwenye visiwa vya Madagascar.

Hayo yamesemwa katika taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo iliyosema kuwa Kimbunga kinachojulikana “ELIAKIMU” kipo eneo la Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Madagascar na kinaelekea Kusini mwa kisiwa hicho.

Aidha, Mamlaka ya hali ya hewa imesema imefuatilia mwenendo wa Kimbunga hicho tangu kilipojitokeza mapema mnamo Machi 15, 2018 majira ya saa 11 asubuhi na kutoa utabiri wa hali ya hewa nchini kwa kuzingatia mifumo yote ya hali ya hewa inayojitokeza.

Hata hivyo, Mamlaka hiyo imesema itajitahidi kutoa taarifa na tahadhari za utabiri kadri inapobidi kufanya hivyo.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Machi 19, 2018
Video: Diamond aachia ngoma mpya na msanii toka majuu ''African Beuty''