Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya maboresho katika ratiba ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/2024 huku ikitaja sababu za maboresho hayo kuwa ni kama kuongeza ufanisi katika michezo ya Ligi na ushiriki wa klabu kwa ujumla.

Aidha maboresho hayo yamezingatia masuala kadhaa yakiwemo kuondolewa kwa klabu za Azam na Singida kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika, ushiriki Young Africans na Simba SC kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika sambamba na ushiriki Simba SC kwenye michuano ya African Football League.

Jambo jingine lililozingatiwa katika maboresho haya ni kutokuwepo kwa michezo ya kuwania Kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), ambayo hadi sasa ratiba yake haijatangazwa na tayari kipindi kilichotengwa kwa michezo ya awali kimepita bila michezo hiyo kuchezwa.

Bodi inaamini maboresho haya yatasaidia kuongeza ushindani miongoni mwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya NBC lakini pia kutoa nafasi kwa wawakilishi wa nchi kwenye michuano ya kimataifa (Young Africans na Simba SC) kushiriki kikamilifu kwenye michuano ya CAF na kupata mafanikio.

Wayne Rooney: Birmingham City itacheza Ligi Kuu
Mikel Arteta kuingia sokoni Januari 2024