Shirika la Reli Tanzania – TRC limeutaarifu umma kuwa limeanza kufanya majaribio ya mabehewa mapya ishirini na mbili (22) ya reli ya zamani (MGR) yaliyonunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma ya usafiri wa abiria nchini kupitia reli ya MGR.

Majaribio yameanza kufanyika kwa kutembeza mabehewa hayo umbali wa kilomita 400 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kurudi Dar es Salaam, baadaye majaribio yatafanyika kwa kutembeza mabehewa kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma na Arusha.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 13, 2022
Uganda mguu ndani, mguu nje CHAN