Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ huenda isishiriki Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ zitakazorindima mapema mwaka 2023 nchini Algeria.

Uganda ilipata tiketi ya kushiriki Fainali hizo kwa kuifunga Tanzania ‘Taifa Stars’ mabao 4-0, baada ya michezo ya nyumbani ya ugenini.

Rais wa Shirikisho la soka Nchini Uganda ‘FUFA’ Moses Magogo amesema huenda kikosi chao kisishiriki Fainali hizo kutokana na ukata wa fedha unaowakabili kwa sasa.

Magogo amesema taratibu za kuhakikisha wanakwenda Algeria kushiriki Fainali hizo zinaendelea kufanywa, lakini nafasi ya kwenda huko ni finyu kutokana na uhalisia wa mambo anaouana kwa sasa.

Taarifa nyingine zinaeleza kuwa tayari Uganda imeshatuma barua CAF ya kujiondoa kwenye Michuano hiyo, ambayo imepangwa kuanza kuunguruma Januari 13 hadi Februari 04 mwaka 2023.

Uganda imepangwa Kundi B lenye timu za DR Congo Ivory Coast na Senegal.

TRC yaanza majaribio mabehewa MGR
Matukio ukatili wa kijinsia yaundiwa mkakati