Vita vya maneno kati ya Marekani na Korea Kaskazini vimezidi kushika kasi kufuatia Rais wa Korea Kaskazini kuendelea na mpango wake wa silaha za nyuklia, kitu ambacho kinapingwa na Marekani.

Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini ilimuita Trump kuwa ‘mchochezi wa vita na mzee’ na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake ya nyuklia kwani inafanya kwaajili ya kujilinda.

Rais Trump alijibu kwa kuandika katika mtandao wake wa kijamii wa Tweeter kuwa, anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini anamuita mzee, kwani pamoja na uzee wake lakini anaongoza taifa lenye nguvu duniani.

Aidha, Trump amesema kuwa hawezi kumuita Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuwa ni mtu’ mfupi na mnene’ ambapo siku chache zilizopita alimuita ni mwendawazi asiyetaka ushauri.

 

Davido anyakua tuzo ya 'MTV EMA'
Ali Kiba, Nandy washinda tuzo za AFRIMA 2017