Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump amefunguliwa mashtaka kutokana na jinsi alivyoshughulikia nyaraka za siri za Serikali, baada ya kuondoka ikulu ya White House na kudaiwa kutumia vibaya nyaraka hizo nyeti za serikali.

Trump alithibitisha habari hizo kwenye ukurasa wa mtandao wake wa True Social, ambapo mawakili wake walimuarifu kuwa wizara ya sheria imemfungulia mashtaka na kwamba ametakiwa kujiwasilisha mbele ya Mahakama ya Miami.

Baadhi ya maafisa wanaofahamu kesi hiyo, wamenukuliwa wakisema kwamba amefunguliwa mashtaka kadhaa ya uhalifu na hatua hiyo inamfanya Trump kuwa rais wa kwanza wa zamani kushtakiwa na Mahakama ya serikali kuu.

Hata hivyo, Mawakili wa Trump hawakujibu mara moja ombi la kutoa maoni kuhusiana na taarifa hiyo. Msemaji wa mwanasheria maalum Jack Smith, ambaye anashughulikia uchunguzi huo, alikataa kutoa maoni yake.

Usiyoyajua kuhusu Wangoni na mgawanyiko wa majina yao
Sudan wamkataa mpatanishi wa Umoja wa Mataifa