Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza mipango yake ya kuzindua mtandao mpya wa kijamii, unaoitwa TRUTH Social.

Trump amesema kuwa jukwaa hilo litakabili ubabe wa makampuni ya teknolojia yanayomiliki mitandao mikubwa ya kijamii.

Aidha Trump Media & Technology (TMTG), pia inakusudia kuzindua mtandao wa video.

Trump alipigwa marufuku na mitandao ya kijamii kama Twitter na Facebook baada ya umati wa wafuasi wake kuvamia majengo ya serikali ya Capitol mwezi Januari.

Fahamu kwanini wanawake wanaenda kanisani kwa wingi
Twiga Stars yaifuata Namibia