Brigedia jenerali, Amirali Hajizadeh wa Jeshi la Kimapinduzi la Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran amesema nchi yake bado ina nia ya kumuua rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Hajizadeh amesema, nia ya kutaka kumuua Trump inatokana na mauaji ya Kamanda Mkuu wa jeshi la Iran, jenerali Qasem Soleimani na lengo lao ni kulipiza kisasi.

Brigedia jenerali, Amirali Hajizadeh wa Jeshi la Kimapinduzi la Jamhuri ya Kiislamu nchini Iran. Picha ya Middle East Eye.

Amesema wanatumai watafanikiwa kumuua Trump na aliyekuwa Waziri wake wa mambo ya nje Mike Pompeo, Jenerali wa zamani wa jeshi la Marekani, Kenneth McKenzie na Makamanda wengine waliotoa amri ya kuuwawa kwa Soleimani.

Iran imekuwa ikirejelea kauli yake ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya Kamanda huyo aliyesimamia operesheni za kigeni, aliyeuwawa kwa shambulio la ndege isiyo na rubani ya Marekani, katika uwanja wa ndege wa Baghdad Januari 2020.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 26, 2023
Ndejembi ataka kasi utatuzi changamoto za Wananchi