Bodi ya Utalii Tanzania inaendelea na mkakati wake wa kupenya katika masoko ya utalii ya Bara la Asia kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii kutoka katika bara hilo pamoja na kuwashawishi watalii kuifanya Tanzania kuwa ni chaguo namba moja la utalii barani Afrika.
Katika maonyesho hayo yanayofanyika Jijini New Delhi nchini India, The Roseate Aero City yametoa fursa kwa wadau wa utalii wa India kuvijuwa vivutio vya utalii vya Tanzania pamoja na kutangaza safari mpya za shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwa kutumia ndege yake aina ya 787-8 Dreamliner mwezi November, 2018.
Aidha, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB, Devota Mdachi amesema kuwa kupitia maonyesho hayo, wadau wa utalii wa India watapata fursa ya kujua kwa kina kuhusu utalii wa Tanzania pamoja na kuweza kufanya biashara na wadau wa utalii wa Tanzania.
“Tunatarajia wadau hao wa India wataitumia ” 787-8 Dreamliner” ya ATCL kwa ajili ya kuwaleta watalii Tanzania, juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania kupitika mashirika haya zitaongeza idadi ya watalii kutoka soko la utalii la India”.
Hata hivyo, Tarehe 19/09/2018 TTB itaendelea na maonyesho hayo katika mji wa Ahmadabad, Crowne Plaza na tarehe 21/09/2018 maonesho yatafanyika mijini Mumbai, Hotel Orchid