Shirikisho la Soka Afrika CAF limewateua waamuzi kutoka nchini Tanzania kuchezesha mchezo wa kufuzu AFCON 2019 Cameroon kati ya Shelisheli na Afrika Kusini utakaochezwa Uwanja wa Stade Linite Oktoba  16,2018.

Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Mfaume Ali Nassoro akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Ferdinand Chacha, Mwamuzi msaidizi namba 2 Alli Kinduru na Mwamuzi wa akiba Elly Sasii. Mtathmini waamuzi anatokea Uganda Ronnie Kalema na Kamishna wa mchezo anatokea France Yves, Jean-Baptiste Etheve.

Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) limemteua Bwana Ahmed Idd Mgoyi kuwa kamishna wa mchezo wa Kufuzu kucheza AFCON 2019 Cameroon, mchezo ambao utazikutanisha Malawi na Cameroon mchezo utakaochezwa Oktoba 16, 2018 Kamuzu Stadium katika Mji wa Blantyre.

Naye Leslie Liunda ameteuliwa kuwa mtathmini Waamuzi mchezo utakaowakutanisha Congo DR na Zimbabwe utakaochezwa Kinshasa Complexe OmniSports Stade Des Martyrs Oktoba 13,2018.

CAF yamtangaza 'Pilato' wa Cape Verde Vs Tanzania
TTB yaipigia chapuo 787-8 Dreamliner kuanza safari ya India