Kukiwa na wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inakaribia kupata ufanisi wa kukamilisha silaha za Kinyuklia, Marekani imepewa onyo la kutoanzisha uchokozi dhidi ya nchi hiyo kwani ipo tayari kulipiza kisasi kwa mshambulio ya Kinyuklia.
”Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nyuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia”.
Taarifa hiyo imetolewa wakati Rais wa nchi hiyo, Kim Jong-un alipohudhuria gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya babu yake, marehemu Kim II-Sung, ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo.
Mtu ammoja anayedaiwa kuwa na uwezo mkubwa katika nchi hiyo amesema kuwa wamejiandaa kwa vita kamili. “tumejiandaa kwa vita kamili” amesema
Aidha, katika gwaride lililofanyika, vifaa vilivyoonyeshwa kwa mara ya kwanza vilikuwa ni makombora ya masafa marefu yanayoweza kwenda kwa takriban kilomita 1000 na nyingina nzito ambapo wachanganuzi wa vifaa vya kijeshi pia wamesema kuwa kuna makombora mawili mapya yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine, lakini haijulikani iwapo yamefanyiwa majaribio.