Baadhi ya Wafanyabiashara sokoni Kariakoo, wamesema kuundwa kwa tume ya watu 14 saba kati yao kutoka kwa wafanyabiashara na saba wa serikalini ikilenga kupitia changamoto walizoziorodhesha kutawezesha kumaliza kero zao ili kufanya kazi huku wakiwa na uhakika.

Wafanyabiashara hao, walimueleza Waziri Mkuu kuwa vitendo vya rushwa vinavyoendekezwa na Mamlaka ya Mapato nchini – TRA na Jeshi la Polisi vinapelekea kuwakimbiza wafanyabiashara wengi nchini.

Wamesema, ukamataji holela inayofanywa na Mamlaka ya Mapato kwa watu wanaoitwa ‘Vishoka’ inawaumiza wafanyabiashara hali inayopelekea kuwadidimiza kiuchumi na kushindwa kufikia malengo yao kitu ambacho si kizuri.

Mara baada ya kusikiliza hoja za wafanyabiashara hao, Waziri Mkuu aliunda tume hiyo ya watu 14 na kusema amevunja kikosi kazi cha Mamlaka ya Mapato nchini – TRA akisema kimekuwa kikifanya kazi bila weledi hivyo kodi zitakusanywa na watu wenye taaluma.

Mahitaji ya Wakimbizi nchini Sudan ni dola bilioni 3
Wizara yaendesha mjadala rasimu ufanyaji biashara