Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) jana jioni alikamatwa na Jeshi la Polisi muda mfupi baaada ya kumaliza mkutano wa hadhara alioufanya jimboni kwake.

Lissu ambaye anakabiriwa na kesi ya uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, aliandika ujumbe kwa wananchi akiwa mikononi mwa polisi, muda mfupi kabla ya kusafirishwa hadi Dar es Salaam.

“Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa na Regional Crimes Officer (RCO) wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander (RPC) Singida nikamatwe apparently (dhahiri) kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam,

 “Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka. It’s likely (inawezekana) nitasafirishwa Dar usiku huu. In fact (hakika) ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Kwa vyovyote itakavyokuwa, there’s no turning back. There’s no shutting up (hakuna kurudi nyuma, hakuna kunyamaza). Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa, whether in freedom or in jail (niwe huru au jela)… Aluta continua!”

Lissu aliandika ujumbe huo kwenye akaunti yake ya Facebook na baadae kusambaa kwa kasi kupitia Whatsap na mitandao mingine.

Afisa habari wa Chadema, Tumaini Makene alithibitisha kukamatwa kwa Lissu akieleza kuwa bado hawajajua sababu za kukamatwa kwake.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alithibisha kutokea kwa tukio hilo huku akikataa kutoa maelezo na sababu zilizopelekea kukamatwa kwa mwanasiasa huyo.

 

Kiwanda Cha Mo Enterprises Chatozwa Faini Ya Milioni Kumi
Akimbizwa hospitali baada ya kukaa ‘Airport’ siku 10 akimsubiri mpenzi aliyempata Mtandaoni