Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa atahakikisha kuwa wabunge wanashirikiana na Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma aliyeapishwa leo katika kutekeleza majukumu yake.
Ameyasema hayo hii leo Ikulu Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma, ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali.
“Sisi kama bunge tunawahakikishia ushirikiano mkubwa sana kwa kuhakikisha kazi za Mahakama zinaendelea kama zilivyo kikatiba na tutaheshimu sana. Yale maneno na makombora ya moja kwa moja ya bungeni ni vitu vya kawaida, ndiyo utamaduni wa bunge,”amesema Ndugai
Aidha, ameongeza kuwa Mahakama ina mchango mkubwa kwa wananchi pamoja na taifa kwa ujumla kwa kuwa hicho ndicho chombo pekee kinachoweza kumtetea mnyonge kuweza kupata haki yake kutoka kwa waporaji.
-
Video: ADC walaani kushambuliwa kwa Lissu
-
Shaka amtembelea Waziri Mkuu Mstaafu, Malecela
-
LIVE IKULU: Rais Magufuli amwapisha Jaji MKuu, Profesa Ibrahim
Hata hivyo, kwa upande mwingine, Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma ameahidi kufanya kazi katika maadili ya kisheria pamoja na kurudisha imani ya wananchi kuhusiana na kupata misaada ya kisheria inayotolewa katika Mahakama mbalimbali ndani ya Tanzania.