Taasisi ya Sweden inayoandaa tuzo za Nobel imesema kuwa mwaka huu haitatoa tuzo hiyo kutokana na kukumbwa na kashfa za ngono miongoni mwa wajumbe wa taasisi hiyo.

Imeelezwa kuwa tuzo hiyo itatolewa mwakani baada ya uamuzi kuafikiwa katika mkutano uliofanyika jijini Stockhom nchini Sweden baada ya kutompata mshindi wa mwaka huu.

Aidha, Katibu wa kudumu wa taasisi hiyo, Anderss Olsson amesema kuwa wameamua kutotoa tuzo hiyo baada ya kuwepo kwa kashfa ya unyanyasaji wa kingono.

“Tunampango wa kutoa tuzo mbili mwakani baada ya jambo hili kutokea katika historia ya tuzo hizi za Nobel kuanzishwa,”amesema Olsson

Hata hivyo, Rais wa bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo Carl-Hendrik Heldin amesema kuwa mzozo uliotokea kwenye taasisi hiyo umeathiri pakubwa utoaji wa tuzo hizo.

Kiongozi wa upinzani akamatwa
Msichana abakwa na kuchomwa moto