Msichana mwenye umri wa miaka 16 nchini India amechomwa moto baada ya wazazi wake kulalamika kwa wazee wa kijiji kuwa binti huyo alibakwa.

Polisi wamesema kuwa wazee wa kijiji waliamuru wanaoshutumiwa kuhusika na ubakaji walipe faini ya rupia 50,000 sawa na pauni 550 kama adhabu.

Aidha, baada ya amri hiyo ya Polisi, watu hao walighadhabishwa na maamuzi hayo na kuamua kuwapiga wazazi wa msichana huyo kisha kumchoma moto binti yao.

”Watuhumiwa wawili waliwapiga wazazi kisha wakakimbilia kwenye nyumba yao wakiwa na washirika wao na kumchoma moto msichana,” Askari Polisi Ashok Ram amesema.

Hata hivyo, Polisi wamesema kuwa binti huyo alibakwa na wanaume wawili katika eneo lenye msitu karibu na kijiji cha Raja Kendua.

Tuzo za Nobel zayeyuka kwa kashfa ya ngono
Video: Aliyegandwa na kiroba asimulia kilichomponza, Vigogo wagongana