Leo Agosti 30 asasi ya kiraia Twaweza imeweka bayana juu ya tafiti iliyofanywa na kuainisha kuwa jijini Dar es salaam kwa 25% muda wa kumsubiri daktari umepunguwa.
Mbali na mafanikio hayo, utafiti huo wa toleo la 19 la Sauti za Wananchi umebainisha kuwa, wananchi sita kati ya 10 (asilimia 61) wanapata huduma za afya katika vituo vya afya vya Serikali, kiwango ambacho kimesalia kama ilivyokuwa mwaka jana.
Ambapo tafiti hizo zimeonesha pia muda wa kusubiri huduma katika vituo vya afya umepungua kidogo kulinganisha na miaka ya nyuma ambayo wananchi saba kati ya 10 walisubiri chini ya saa moja mwaka 2014.
Mwaka 2014, idadi ya wananchi waliokuwa wakipata huduma za afya kwenye vituo vya umma ilikuwa ni takriban watano kwa kila 10 sawa na asilimia 45.
-
Msigwa alalamikia Serikali awaombea kifuta jasho wenye vyeti feki
-
Mdee alia na polisi, asema kuna matapeli wanamsumbua
Utafiti huo uliohusisha sampuli ya wananchi 1,801 unaeleza kuwa, ni asilimia 16 hadi 20 ya waliohojiwa huenda hupata matibabu kwenye vituo vinavyomilikiwa na watu binafsi, makanisa au mashirika yasiyo ya kiserikali.