Nchini China kocha mpya wa klabu ya ‘Shanghai Shenhua’ Wu Jingui ametuhumu mshambuliaji wa klabu hiyo Carlos Tevez kuongezeka uzito na kusema kuwa hatampanga katika kikosi chake mpaka hapo atakapo punguza uzito.
Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alijiunga na klabu ya Shanghai Shenshua kwenye ligi ya China mwaka jana mwezi Desemba akiwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani.
Pamoja na Tevez kuwa analipwa mshahara wa pauni 610,000 kwa wiki mshambuliaji huyo ameshindwa kuonyesha makali yake akiwa amefunga mabao mawili tu katika michezo 15 aliyoichezea klabu hiyo.
Tevez ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara amekuwa akijitahidi kumshawishi kocha Jingui aliyechukua nafasi ya Gus Poyet mapema mwezi Septemba lakini kocha huyo amesema hatamjumuisha Tevez katika kikosi chake mpaka pale atakapoonyesha kiwango cha kuridhisha.
-
Rufaa ya Sadio Mane yagonga ukuta
-
Edinson Cavani avunja rekodi ya Ibrahimovic
-
Ederson aibuka mazoezini na vazi la Petr Cech
”Nitamtaarifu kuhusu mbinu zangu lakini sitamuita kikosini kwani hayuko tayari kimwili kwa sasa hayuko tayari kucheza” alisema Wu.