Mabingwa wa Dunia mara nne timu ya taifa ya Ujerumani, watakutana uso kwa macho na England kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora katika Fainali za UEFA Euro 2020, zinazoendelea kwenye miji mbalimbali Barani Ulaya.
Ujerumani ambao kwa mara ya mwisho walitwaa ubingwa wa Dunia mwaka 2014, wametinga harua ya 16 Bora, baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Hungury, kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi F, uliochezwa usiku wa kuamkia leo mjini Munich, Uwanja wa Allianz Arena.
Hungary walitangulia kupata bao dakika ya 11, kwenye mchezo huo uliokua na vuta nikuvute kupitia kwa Adam Szalai anayeitumika klabu ya Mainz, inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).
Andras Schafer aliifungia bao la pili Hungary dakika ya 68, baada ya Kai Havertz kuisaiwazishia Ujerumani dakika ya 66 na Leon Goretzka akafunga bao la pili lililowanusuru dakika ya 84.
Sare hiyo inaifanya Ujerumani kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi F, na ni dhahir inakwenda kukutana na vijana wa kocha Gareth Southgate, kwenye Uwanja Wembley mjini London, siku ya Jumanne.
Michezo mingine ya hatua ya 16 Bora ya UEFA Euro 2020.
26 Juni 2021
Wales Vs Denmark (Johan Cruyff Arena) Amsterdam
Italy Vs Austria (Wembley Stadium) London
27 Juni 2021
Uholanzi Vs Jamuhuri ya Czech (Puskás Aréna) Budapest
Ubelgiji Vs Ureno (La Cartuja) Seville
28 Juni 2021
Croatia Vs Hispania (Parken Stadium) Copenhagen
Ufaransa Vs Uswiz (Arena Națională) Bucharest
29 Juni 2021
Sweden Vs Ukraine (Hampden Park) Glasgow