Timu ya taifa ya Ufaransa imepata matokeo ya kushangaza katika mchezo wa kuwania kushiriki katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi baada ya kutoka suluhu ya 0-0 na timu ya taifa ya Luxembourg inayoshika nafasi ya 136 katika viwango vya FIFA duniani.

Ufaransa iliyopata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Uhoranzi siku ya Alhamisi ilimiliki mpira kwa asilimia 76 katika mchezo huo na kupiga mashuti 34 lakini ilijikuta ikishindwa kupata ushindi dhidi ya Luxembourg.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ufaransa kushindwa kuifunga Luxembourg tangu mwaka 1914. Ufaransa bado inaongoza Kundi ‘A’ ikiwa mbele kwa pointi moja tu zaidi ya Sweden wanaoshika nafasi ya pili katika kundi hilo.

Kikosi cha Ufaransa kinachonolewa na kocha Didier Deschamps  kiliundwa na wachezaji wakali akiwemo kiungo wa Manchester United Paul Pogba, Mshambuliaji waAtletico Madrid Antoine Griezmann na Kylian Mbappe amabaye kwa sasa amejiunga na klabu ya Paris St-Germain kwa mkopo akitokea katika klabu ya Monaco.

Wachezaji wa Luxembourg wakishangilia baada kutoka suluhu na Ufaransa

”Matokeo ya Alhamisi yaluwa mazuri na leo tulihitaji kupata pointi tatu,tutazidi kupambana mpaka mwisho japo matokeo ya leo hayaridhishi” alesema kocha wa Ufaransa Didier Deschamps.

 

 

Kweli Arsenal wana mkosi, Sanchez aumia tena
Video: Saida Karoli awaweka katika 'Kichaka' Belle 9 na G Nako