Harakati za kuwasaka wabadhirifu wa fedha za umma ili waingie kwenye msululu wa oparesheni ya kutumbua majipu iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya tano zimeibua tuhuma nyingine zinazomhusu mmoja kati ya vigogo anayedaiwa kuwa mfanyakazi wa Ikulu.

Taarifa zilizochapishwa katika gazeti la MwanaHalisi zinaeleza kuwa uchunguzi uliofanywa na gazeti hilo umebaini nyaraka zinaoonesha kigogo huyo alitumia fedha za walipa kodi kiasi cha shilingi 821,997.24 kwa ajili ya kufanyiwa huduma ya kukandwa mwili (massage), katika hoteli ya kifahari ya Four Seasons Safari Lodge iliyoko ndani ya mbuga za wanyama za Serengeti, Arusha.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, stakabadhi waliyoipata katika hoteli hiyo ilionesha kuwa kigogo huyo alifika hotelini hapo April 17 mwaka huu tarehe ambazo Rais mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa na ziara jijini Arusha.

Imeelezwa kuwa kigogo huyo ambaye hoteli hiyo haikutaka kumtaja jina alilala katika chumba namba 9017 na alikuwa na mrembo wake ambaye kwa pamoja walipata huduma zilizoingizwa kwenye stakabadhi iliyolipiwa na Ikulu. Mbali na huduma ya Massage, huduma nyingine zilizoorodheshwa katika nakala ya ankara hiyo ni usafi wa nguo ambao uligharimu shilingi 676,000.

Katika kutafuta kujiridhisha, gazeti hilo lilimpigia simu afisa wa hotel ya Four Seasons Safari Lodge ambaye licha ya kukataa kutoa maelezo alikiri kuwapokea baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu katika siku tajwa.

Haji Duni Kubaki Chadema au Kurejea CUF? Mwenyewe Ajibu
MC Azua Kizaazaa baada Kumvisha Taji La 'Miss Universe' Kimakosa Mrembo ambaye hakushinda