MC wa shindano la urimbwende la ‘Miss Universe 2015’, Steve Harvey alizua taharuki na vilio ukumbini baada ya kumtangaza kimakosa mrembo wa Colombia, Ariadna Gutiérrez kuwa mshindi wa taji hilo badala ya Mrembo wa Ufilipino, Pia Alonzo Wurtzbach aliyeshinda kihalali.

Harvey

Wakati ukumbi ukisubiri kwa hamu kusikia jina la mshindi wa taji hilo lililokuwa kwenye kadi iliyofungwa, MC alilisoma kwa mbwembwe jina la Miss Colombia kuwa ndiye mshindi na kuwafanya mashabiki wake washangilie huku waandaaji wakichanganyikiwa nini kimetokea.

Hata hivyo, furaha hiyo iligeuka baada ya MC kulazimika kuomba radhi baada ya kuelezwa na waandaaji kuhusu makosa hayo. Mwisho alimtaja mshindi halali ambaye ni mrembo wa Ufilipino, hali iliyozimisha furaha na vilio vya awali.

Miss Universe 2015

“Okay folks, I have to apologize. The first runner-up is Colombia,” In other words, Miss Universe 2015 is actually Miss Philippines Pia Alonzo Wurtzbach!,” MC alisawazisha makosa.

Ufisadi: Kigogo Adaiwa Kutumia Fedha Za Umma Kufanya 'Masaji' Na Mrembo Wake
Picha: Mrembo wa Hispania ashinda taji la Miss World 2015