Mrembo wa Hispania, Mireia Lalaguna Royo mwenye umri wa miaka 23 ametangazwa kuwa mshindi wa taji la Mrembo wa dunia (Miss World 2015).

Mireia ambaye ni mwanamitindo maarufu kutoka Barcelona, alifanikiwa kuwafunika warembo wenzake waliokuwa wanapewa nafasi zaidi huku mrembo wa Uingereza akishindwa kugusa hata orodha ya ‘top 10’.

CHINA-LIFESTYLE-MISS WORLD-PAGEANT

Mrembo huyo aliwavutia watu wengi hasa baada ya kutoa majibu yenye maneno mazito. Moja kati ya sentensi zilizowavuta wengi ni pale aliposema, “mimi kuwa mzuri nje haimaanishi kuwa hata ndani pia ni mzuri”.

Nafasi ya pili ilienda kwa Mrembo wa Urusi, Sofia Nikitchuk, na nafasi ya tatu ilienda kwa mrembo wa Indonesia.

Naye Mrembo wa Tanzania, Lilian Kamazima alifanikiwa kuingia kwenye ‘top ten’ ya Miss World Beauty with a Purpose’.

Lilian Kamazima

MC Azua Kizaazaa baada Kumvisha Taji La 'Miss Universe' Kimakosa Mrembo ambaye hakushinda
FC Barcelona Bingwa Wa Soka Duniani