Mchungaji wa Kanisa la New Life Prayer Centre, Ezekiel Odero amesema uamuzi wa Serikali wa kufuta usajili wa kanisa lake hauna mashiko na ni njama ya kuzuia kuendelea kwa kanisa hilo.

Katika ombi lililowasilishwa katika mahakama ya Milimani, Mchungaji huyo anasema hakuwa na habari kwamba alifaa kuwasilisha taarifa kwa msajili wa vyama kueleza ni kwa nini kanisa lake lisifungwe na kwamba alijua agizo hilo kupitia vyombo vya habari siku 8 baada ya muda kukamilika.

Wiki iliyopita, Serikali nchini Kenya ilitangaza kuyapiga marufuku Makanisa matano likiwemo lile la mshukiwa wa mauaji ya Shakahola, Paul Mackenzie la Good News International Ministries, kuanzia Mei 19, 2023.

Aidha, marufuku hiyo pia iliyakumba makanisa mengine manne huku Mhubiri Ezekiel Odero ambaye anahusishwa kushirikiana na Mackenzie akidaiwa kuchunguzwa kwa mashtaka kadhaa ikiwemo mauaji, itikadi kali na utakatishaji fedha.

Tanzania, Comoro kushirikiana Sekta za Afya, Uchukuzi
Askofu Shoo akubali uwekezaji, akataa kuwagawa Watanzania