Serikali imepanga kuanza kufanya minada ya korosho na ufuta kwa njia ya kielektroniki kuanzia msimu ujao ili kuongeza thamani ya zao la Korosho na Ufuta.
Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti aliyetaka kujua ni njia zipi zinatumiwa na Serikali katika kudhibiti mporomoko wa bei katika Soko la Dunia na kusababisha Wakulima kupata hasara
Bashe amesema mpango huo pia utakwenda sawia na kutoa elimu kwa Wakulima ili kuzingatia ubora wa Korosho zisizokuwa na unyevu kwa kuwa zenye unyevu zimekuwa zikirudishwa kwa Wakulima na kuzua malalamiko mengi kutokana na Korosho hiyo kuharibika kabla haijafika sokoni.