Kaimu Kocha Mkuu wa Young Africans Juma Mwambusi ameahidi kufanya marekebisho ya kifundi kwenye kikosi chake, kabla ya mchezo wa mzunguuko wa 26, ambao utashuhudia wakicheza dhidi ya Biashara United Mara mwishoni mwa juma hili, Uwanja wa Benjamin Mpaka jijini Dar es salaam.

Mwambusi ametoa ahadi hiyo baada ya kikosi chake kulazimisha sare ya bao 1-1 na KMC nyumbani, Jumamosi (April 10), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha huyo amesema hakutegemea kushuhudia matokeo hayo kwenye mchezo dhidi ya KMC FC, lakini hana budi kukubalina nayo, na kuyachukua kama sehemu ya kuanzia kwenye maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Biashara United Mara inayofunga safari kutoka mjini Musoma mkoani Mara, tayari kwa mchezo huo.

Mwambusi amesema: “Hayakuwa mategemeo yetu kupata matokeo yale lakini ndivyo mpira wa miguu ulivyo, baadhi ya wachezaji hawakuwa katika kiwango tulichotegemea jambo lililotukosesha alama tatu muhimu,” alisema Mwambusi na kuongeza

“Nimeona matatizo hayo, tunarudi kwenye uwanja wa mazoezi kufanyia marejeo na masahihisho na kuhakikisha kila nafasi tutakayoitengeneza inatumiwa vizuri na kutupa matokeo chanya,”

Matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya KMC FC yameendelea kuiwekea Young Africans kwenye mazingira magumu ya kutwaa ubingwa msimu huu, huku ikifikisha alama 51, ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 47, Simba SC inashika nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 46.

Ajinyonga baada ya kukataliwa na mpenzi
Serikali yawapatia ufumbuzi wakulima wa Ufuta, Korosho