Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza msururu wa masharti mapya ya kupambana na ongezeko la visa vya virusi vya Corona nchini humo, ambapo sharti mojawapo ni lakutotoka nje.
Wakati akilihutubia Taifa Rais Museven amesema kuwa usafiri wote wa kibinafsi na wa umma nchini humo umepigwa marufuku kwa siku 42 zijazo isipokuwa kwa huduma muhimu na mizigo.
Aidha Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebbe pamoja na mipakani kutabakiwa kwaajili ya watalii na wale wanaorejea nchi humo, ambapo mamlaka zimepewa jukumu la kuhakikisha kuwa hakuna kesi mpya ya Covid Nchini humo.
Hata hivyo amri ya kutoka nje imesogezwa kutoka saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja na njsu alfajiri, ambapo wafanyabiashara ya bodaboda wametakiwa kubebe bidhaa tuu.
Kazi zote zinazozingatiwa sio za lazima, shule na taasisi za kujifunzia, sehemu za ibada, na hafla za michezo pia zimefungwa kwa siku 42 zijazo.
Museveni amesema, hatua hizo ni muhimu kukomesha maambukizi ya sasa ya kijamii na kupeuka kuulemea kabisa mfumo wa utoaji wa huduma za afya.
Katika siku kumi na mbili zilizopita tu, nchi hiyo ilirekodi visa 15 800 na vifo 190 vinavotokana ana Corona.