Makatibu wa afya nchini wametakiwa kusimamia nyenzo na rasilimali za kuendeshea huduma za afya zilizopo kwenye maeneo yao ya kazi kama ilivyo kwenye majukumu yao kwani wao ni kioo na alama ya uendeshaji wa taasisi.

Hayo yamesemwa leo Juni 18, 2021na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa kufungua mkutano wa mwaka wa Chama Cha Makatibu wa Afya Tanzania ( AHSATA) unaofanyika mkoani Morogoro.

Amesema, Makatibu wa afya lazima waelewe vizuri majukumu yao ili kuweza kusimamia na kuendesha taasisi zao vizuri na hatimaye kupata mafanikio kwani wao ndio watendaji wakuu katika kusimamia mifumo ya afya .

“Tunataka mifumo imara ya afya na kuthamini jinsi Serikali ilivyowekeza kwenye mifumo hii ya afya” amesema Dkt. Gwajima.

Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “Uimarishaji wa mifumo ya afya ni nguzo muhimu katika usimamizi wa rasilimali za sekta ya afya nchini”

Aidha, Dkt. Gwajima amesema anatambua kada hiyo ndio pekee haina kurugenzi wizarani, hivyo ameagiza hilo lifanyiwe kazi ya uchambuzi kuona kuna kipingamizi gani kinachozuia hilo iwapo ni jambo lenye tija

‘’Lazima tubadilike na tuondoe dhana ya uongozi kwenye afya lazima mtu awe kada ya utabibu ‘Medical Doctor andaeni kongamano litakalojadili hili,kwani mimi nilipokuwa DMO hata RMO nilifanikiwa kwa kusaidiwa na kada zingine,hivyo Muuguzi au taaluma nyingine ya afya anaweza kuongoza taasisi ya afya maana huo ni uongozi na siyo kazi ya taaluma maalumu’.

Aidha amewataka waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwapatia fursa na uhuru wenye kuzingatia sheria makatibu wa afya.

Metacha Mnata aomba radhi
Mama Mkude afunguka sakata la Simba SC