Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia kesi ya uhujumu uchumi na kuwaachia huru wafanyakazi sita wa kampuni ya meli ya Sinota Shipping Company waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu

Hakimu Mkazi mwandamizi, Rashid Chaungu amefuta mashtaka hayo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania( DPP) kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.

 Washtakiwa hao ambao wote ni raia wa China ni Jin Erhao (35), Chengfa Yang (49), Ren Yuangqing (55), Shu Nan (50), Chen Shinguang (45) na Gu Jugen (57) wote wakazi wa mtaa wa Sokoine, Ilala jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa baada ya kuachiwa walitoka mahakamani huku wakikimbia na kupanda gari kisha kuondoka.

Wakili wa Serikali, Kija Luzugana ameieleza mahakama hiyo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

“Hakimu washtakiwa wote wapo mbele ya mahakama hii na DPP amesema hana nia ya kuendelea na shauri hili,”  amedai Luzugana.

Mara baada ya waakili huyo kuipa taarifa hiyo Mahakama, Hakimu Chaungu amesema washtakiwa wamefutiwa mashtaka yao na kuachiwa huru.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 57/2020, washtakiwa walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matatu yaliyowafanya wakose dhamana.

Katika shtaka la kwanza wanadaiwa Agosti 11, 2020 mtaa wa Sokoine kwa pamoja na kwa makusudi walisimamia genge la uhalifu lililopelekea kupatikana kwa ndege  huyo mwenye thamani ya Sh1,150,000.

Azam FC: Tutaishusha Young Africans
Zrane: Kagere bado anahitajika