Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake wamefikishwa kwa mara nyingine tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kujibu mashtaka yanayowakali.

Sabaya alifika mahakamani hapo leo asubuhi Juni 18, 2021 akiwa katika basi la  Magereza huku watu waliofurika mahakamani hapo wakimzomea.

Kwa mara ya kwanza Sabaya na wenzake walifikishwa Mahakamani Juni 4, 2021, na kusomewa mashtaka matano ambayo ni pamoja na uhujumu uchumi na kuongoza magenge ya uhalifu.

Mkuu huyo wa wilaya wa zamani alishuka kwenye gari akiwa amevaa suti ya bluu mkononi akiwa ameshika vitabu huku uso wake ukiwa na tabasamu licha ya zomeazomea kutoka kwa watu waliokuwepo mahakamani hapo.

Sabaya alijipatia Sh90 milioni kutoka kwa mfanyabiashara, Francis Mroso mkazi wa kwa Mromboo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.

Pia, Sabaya na walinzi wake wawili, Sylivester Nyengu (26) maarufu kicheche na Daniel Mbura (38) wanakabiliwa na  makosa mawili ya ujambazi wa kutumia silaha wakidaiwa kuyatenda Februari 9, 2021.

Mama Mkude afunguka sakata la Simba SC
Azam FC: Tutaishusha Young Africans