Serikali ya Zambia imetangaza kipindi cha siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa zamani Kenneth Kaunda, hayati kaunda alifariki Juni 17, katika hospitali ya jeshi mjini Lusaka akiwa na umri wa miaka 97.

Viongozi mbalimbali wameonyesha hisia zao kupitia mitandao ya kijamii kumuelezea hayati Kenneth Kaunda, Kupitia mtandao wa Facebook Rais wa sasa wa Zambia Edgar Lungu amemsifu hayati Kaunda akimtaja kuwa shujaa wa kweli wa kiafrika.

Pia Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson naye ametuma salamu za rambirambi kwa taifa la Zambia akisema kupitia ujumbe wa Twitter kuwa amesikitishwa na kifo cha Kaunda.

Kaunda alipigania ukombozi wa nchi yake kutoka ukoloni wa Waingereza hadi uhuru ulipopatikana mwaka 1964 na kuwa Rais wa kwanza wa Zambia huru.

Wakati wa utawala wake wa miaka 27 hayati Kaunda alisifika kwa kupendelea njia za amani kutatua mizozo na kusaidia harakati za ukombozi wa mataifa ya kusini mwa Afrika.

Tanzania yazidi kung'ara uwekezaji
Papaa Msofe afutiwa mashtaka aachiwa huru