Kufuatia Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kutangaza vifo vya takriban wanajeshi 54 waliouawa katika shambulizi dhidi ya kambi ya kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika iliyokuwa ikishikiliwa na wanajeshi wa Uganda Mei 26 nchini Somalia Taifa hilo limekuwa katika simanzi na maombolezo.
Hatua ta kutangaza vifo hivyo, sasa inamaliza minong’ono ilikuyokuwa imetawala hapo awali baada ya Museveni kusema kumetokea vifo vya Waganda bila kutoa maelezo zaidi kuhusu Wanajeshi hao, wanaohudumu katika Kikosi cha mpito cha Umoja wa Afrika Nchini Somalia – ATMIS.
“Tulirekodi hasara kubwa, maiti za wanajeshi 54 walioangamia, akiwemo mmoja wa makamanda wa kikoi hicho,” alieleza Rais Museveni kupitia taarifa yake iliyochapishwa kwenye ukurasa wake rasmi wa Twitter huku Waganda wengi wakisema wameshitushwa na taarifa hizo mbaya.
Kikosi hicho cha walinda amani chenye Wanajeshi 22,000, kimekuwa kikitoa msaada kwa Serikali ya Somalia katika kupambana na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Al-Shabab, tangu Mwaka 2022 ilipochukua nafasi ya Misheni ya AU Nchini Somalia – AMISOM.