Mtu mmoja mwenye majeraha, aliyeonekana katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Roma akiwa mtupu kwenye madhabahu kuu akidai kupinga vita vya Ukraine.

Akithibitisha tukio hilo, mpatanishi wa shirika amesema nyuma ya mtu huyo kulikuwa na maandishi yanayoita kuokoa watoto wa Ukraine na majeraha ya mwilini kwake yalikuwa ya mikwaruzo.

Hata hivyo, walinzi wa Vatican walimkabidhi mwanamume huyo ambaye bado haijafahamika utambulisho wake kwa Polisi wa Italia.

Tukio hilo limetokea muda mfupi kabla ya kufungwa kwa kanisa kuu Juni Mosi, 2023 na vyombo vya Habari kadhaa vya Italia vilichapisha picha za tukio hilo.

Ajali za barabarani: Polisi msimamo wenu unawapa lawama - RSA
Mtibwa Sugar: Tunazitaka alama zote sita